Monday, 14 August 2017
Jeshi la Uganda lasema halina mpango wa kuingia Kenya

Jeshi la Uganda UPDF limekanusha taarifa kuwa liko tayari kuingia nchini Kenya kusaidia kudhibiti hali ya usalama nchini humo baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi, huku mpinzani wake mkuu Raila Odinga akiyapinga matokeo hayo.
Waziri wa mawasiliano nchini humo Frank Tumwebaze amesema jeshi la Uganda haliwezi kutumwa nje kushiriki operesheni ya kijeshi kisiri.
Msemaji wa jeshi la Uganda Richard Karemire, kupitia taarifa, amesema Kenya ni nchi huru na usalama wake umo chini ya serikali ya nchi hiyo.
Aidha, amesema Uganda haijapokea ombi kutoka kwa Kenya kutuma majeshi yake nchini humo au kuomba usaidizi.
Polisi Watangaza Kiama Kwa Wapiga Debe Dar Es Salaam


Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dares salaam limetangaza oparesheni maalum katika vituo vyote vya daladala siku ya Jumatatu kwa ajili ya kuwaondosha wapiga debe.
Uamuzi huo unafuatia kushamiri vitendo vya wizi na uporaji wa mali za abiria katika vituo vya daladala vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojulikana kwa jina la wapiga debe.
Kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lucas Mkonya amesema wananchi wengi wamekua wakipeleka malalamiko juu ya wizi huo unaotokea kwenye vituo vya daladala unaofanywa na baadhi ya wapiga debe kwenye vituo.
Ni matumani ya wananchi kuwa Operesheni hiyo itazaa matunda kufuatia kukithiri vitendo vya wizi vinavyofanywa na wapiga debe ambao asilimia kubwa ni mateja.
Utafiti wa mtandao huu unaonesha kuwa wezi wamekua wakishirikiana na baadhi ya makondakta wa daladala kuwaibia abiria.
Wezi wamekua wakipanda katika daladala na kuiba kisha kushuka bila kutozwa nauli na makondakta suala linaloashiria kuwa wanafahamiana.
Subscribe to:
Posts (Atom)