Thursday, 31 August 2017

Ridhiwani‘Amshukia’ Waziri Kigwangalla Kuhusu Uchochezi


ridhiwani
IMG-20170426-WA0006

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amemvaa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala na kumwambia anaweza kuwa sehemu ya wachochezi kwa anachokifanya.

Ridhiwani Kikwete amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa twitter baada ya Mhe. Kigwangalla kuonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma katika kuwafanyia usaili baadhi ya watu waliojitokeza kwenye usaili wa ajira iliyotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao umefanyika mapema jana, Agosti 30, 2017.

“Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakuwa sehemu ya wachochezi! Mhe. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lakini picha inatoa jibu sahihi,” aliandika Ridhiwani katika ‘post’ ya Kigwangalla.

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jana Agosti 30, 2017 ilifanya usaili kwa ajili ya nafasi za kazi katika Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo takribani watu 30,000 walijitokeza huku ikiwa watu 400 pekee ndiyo wanaotakiwa huku picha za maelfu ya watu hao zikiwa zinazagaa katika mitandao ya kijamii na kuzua majadiliano makubwa.

RAIS MAGUFULI ASITISHA BOMOABOMOA YA NYUMBA ZAIDI YA 300

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
IMG-20170426-WA0006

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Rais Magufuli amesitisha zoezi la bomoabomoa la nyumba zaidi ya 300.

Nyumba hizo ni zile zilizojengwa katika Bonde la Makamba, Kata ya Tuangoma, Wilayani Temeke.

“Serikali imesisitiza kuwa zoezi hilo linapaswa kufanywa kwa kufuata taratibu na sheria,” amesema. 

Hivi karibuni, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilitangaza Bomoa Bomoa nchi nzima kwa wananchi waliovamia na kujenga kando ya Mito na Bahari ikiwa ni siku chache baada ya kucha vilio maeneo kadhaa ikiwemo pembezoni mwa Barabara ya Morogoro eneo la Kimara na kuwaacha baadhi ya watu bila makazi.

Akizungumza Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche alisema wananchi waliofanya makazi katika maeneo hayo wanapaswa kuondoka kabla ya kuvunjiwa kwa nguvu.

Bodi Ya Mikopo Yaongeza Muda Wa Kuomba Mikopo.

008.CHUO_-620x308
IMG-20170426-WA0006
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imeongeza muda wa maombi ya kuomba mkopo kwa wanafunzi wa mwaka wa masomo wa 2017/2018.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, wanafunzi wa elimu ya juu sasa wataweza kuomba mkopo hadi kufikia Septemba 11, ikiwa ni siku saba mbele ya iliyokuwa tarehe ya mwisho hapo awali ya Septemba 4, mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema hadi kufikia jana, jumla ya waombaji 49, 282 wamekwishaingiza taarifa zao katika mtandao wa HESLB kwa ajili ya kuomba mkopo.

clouds stream