Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Rais Magufuli amesitisha zoezi la bomoabomoa la nyumba zaidi ya 300.
Nyumba hizo ni zile zilizojengwa katika Bonde la Makamba, Kata ya Tuangoma, Wilayani Temeke.
“Serikali imesisitiza kuwa zoezi hilo linapaswa kufanywa kwa kufuata taratibu na sheria,” amesema.
Hivi karibuni, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lilitangaza Bomoa Bomoa nchi nzima kwa wananchi waliovamia na kujenga kando ya Mito na Bahari ikiwa ni siku chache baada ya kucha vilio maeneo kadhaa ikiwemo pembezoni mwa Barabara ya Morogoro eneo la Kimara na kuwaacha baadhi ya watu bila makazi.
Akizungumza Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche alisema wananchi waliofanya makazi katika maeneo hayo wanapaswa kuondoka kabla ya kuvunjiwa kwa nguvu.