Thursday, 9 November 2017

Papa Francis apiga marufuku uuzaji wa sigara Vatican

Licha ya sigara kuiletea mamilioni ya fedha Vatican ,papa Francis amesema kuwa hawezi kuruhusu binaadamu kuathiriwa kiafyaLicha ya sigara kuiletea mamilioni ya fedha Vatican ,papa Francis amesema kuwa hawezi kuruhusu binaadamu kuathiriwa kiafya

Papa Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao.

Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.

Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei .

Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya yuro kila mwaka.

Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.

Mtoto amvua kofia Papa Francis

Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.

''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema.

''Ni kitu ambacho ni lazima kufutilia mbali licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa''.

Papa Francis ambaye pafu lake moja liliondolewa wakati alipokuwa kijana havuti sigara.

Wafanyikazi wa vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka lisilotozwa ushuru.

Aliyedaiwa Kununua Nyumba Za Lugumi Akamatwa Na Polisi



Moja ya nyumba hizo za Lugumi.



Mtu aliyedaiwa kujitokeza leo na kufanikiwa kununua nyumba mbili za Mfanyabiashara, Said Lugumi, Dkt. Luis Shika amekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kushindwa kutoa asilimia 25 ya fedha kama yalivyo masharti ya mnada. Mnada huo sasa unarudiwa tena muda huu.

Awali mtu huyo aliyefika mnadani hapo akiwa amevaa suruali, shati, tai na makobazi (sandals) alidaiwa kufanikiwa kununua nyumba hizo mbili za Mfanyabiashara, Said Lugumi zilizopo Mbweni, Jijini Dar es Salaam kwa Shilingi Bilioni 1.1 na Shilingi Milioni 900 kupitia kampuni ya udalali ya Yono.

Nyumba hizo zinauzwa kwa njia ya mnada kufuatia deni alilokuwa akidaiwa Lugumi na Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo katika mnada wa awali nyumba hizo zilikosa wateja kutokana na bei yake kuwa juu sana.


Dkt. Luis Shika.

Rais Magufuli Awasili Uganda Kwa Ziara Ya Siku 3





Rais, Dkt. John Pombe Magufuli leo amewasili nchini Uganda kwa ziara ya siku 3 kwa mwaliko wa Rais, Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kukamilisha siku 4 za ziara yake Mkoani Kagera.

Kwa pamoja, marais hao wataweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Bomba la kusafirishia Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga, Tanzania.

clouds stream