Tuesday, 1 April 2014

MAMBO YA KUFIKIRIA KABLA YA KUCHAGUA GAUNI LA HARUSI.


Kuchagua gauni la harusi inaweza kua kitu kigumu na cha kukupa mawazo sana na maswali mengi kichwani. Unaweza kujiuliza maswali mengi kama " je, mpenzi wangu atalifurahia?, Familia yangu nayo itafurahia, gauni linaweza kugharimu kiasi gani? Je litaendana na aina ya harusi ninayo itaka? na mambo mengi kama hayo. Naomba nikutoe shaka kidogo kuhusu hili swala, kuna vitu vichache sana vya muhimu vya kuangalia. jaribu kukaa katika muongozo huu:

1. KUA NA MAWAZO CHANYA JUU YAKO BINAFSI.

Siku zote ukianza kufikiria kua unaenda kutafuta gauni la harusi ukiwa na mawazo ya kua hutopata gauni sahihi kwaajili yako basi ujue kua unajinyima mwenyewe uwezo wa kupata gauni zauri. Mara nyingi waswahili husema, aliwazalo mjinga ndilo litakalomtokea, ukiwaza kua hutapata kilichobora kabla hata ya kuanza kutafuta basi itakula kwako. Fikiria kwa upana na hata ukiona kua bado hujapata chaguo sahihi usijipe mawazo mabaya kwani sehemu na machaguo yako mengi.

2. TUMIA MUDA WAKO VIZURI KUTAFUTA GAUNI.

Dunia imebadilika sana siku hii. Mitindo mingi sana ya magauni ya harusi yako mitandaoni, kwenye magazeti, kwenye majarida na hata kwenye baadhi ya vioindi vya televisheni. Jitahidi kua na picha kichwani ya aina ya gauni unalohisi kua ni sawa kwako ili uweze kujiletea uwezo mzuri wa kuchagua. Wakati wote huu pia ujitahidi kuhusisha watu wanaohusika na harusi yako kama mpanbe wako au mshauri.

3. TAFUTA KINACHOKUVUTIA ZAIDI KATIKA GAUNI.

Mara nyingi mtu hujua kitu kinachomvutia sana kutoka na majaribio. Ukijaribu na kujaribu utajua baadhi ya vitu ambavyo vinaugusa moyo wako katika gauni. Ukishajua hivo basi utakua umepunguza uwanja wa magauni ya kutafuta na kupata kile kinachokuvutia zaidi.

4. JARIBU KUTIZAMA BAJETI YAKO.

Wabongo wanasema, mipango sio matumizi. Kila mara ni vyema kujua kamati yako imepanga bei gani kwaajili ya gauni. Unaweza chagua kitu ambacho kiko mbali sana na uwezo wako kifadhe na baada ya hapo kujikuta ukipata simanzi. Jitahidi kufanya makisi mazuri ya pesa iliyopo ili ujitahidi kupata kitu kizuri kinachoendana na dhamani yake.

5. CHAGUA MTU SAHIHI WA KUCHAGUA NAE NGUO.

Mara nyingi kama binadamu kuna hali flani ya kukubali au kukataa ushauri wa mtu na pia ushauri unatofautiana. Ukiamua kuchagua gauni la harusi chagua mtu ambae anweza kukupa ukweli na ambae sio muoga kusema kua hii haijakupendeza. Ukipata mtu wa ndio tu basi unaweza kujikuta sio katika harusi.

6. JUA MADUKA YA VIFAA VYA BIBI HARUSI NA UPAMBAJI WAO.

Kuna baadhi ya sehemu wamekariri jinsi ya kumpamba bibi harusi na sio kumpamba kutokana na jinsi alivyo. Kutokana na hayo inabidi uangalie baadhi ya picha walizopamba watu na uweze kutofautisha na kutizama kama kuna hali ya kufanana sana. ukiona ufanano umezidi jua kua hautafanyiwa kitu cha tofauti sana. Jaribu pengine na pengine tena.

7. ENDELEA KUWA NA MAWAZO CHANYA.
Ukiwaza vyema utapata mema, jaribu kujiweka katika hali ya kua wazi na kupokea mawazo kwa watu mbali mbali lakini usipoteze lengo. Kua mchangamfu, cha muhimu jua kua unapendwa.

clouds stream