Monday 14 April 2014

AZAM BINGWA


Kilabu ya Azam FC ya Dar es Salaam iliyopanda Ligi kuu Tanzania Bara miaka sita iliyopita,hatimaye imetwaa Ubingwa wa soka Tanzania bara hapo jana baada ya kuilaza Mbeya City bao 2-1 .
Kwa Matokeo hayo Azam imefikisha Pointi 59 ambazo hazitaweza kufikiwa na Timu ya Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa pointi 55 kwa sasa hata kama itashinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Simba hapo Jumamosi ijayo.
Kwa Ushindi huo wa Kihistoria kwa Azam,imepata uwakilishi wa Tanzania kwenye Michuani la Klabu Bingwa barani Afrika msimu ujao huku pia ikifuta mtindo wa miaka mingi uliozoeleka ambao Timu za Simba na Yanga ndizo zilikuwa zikipokezana Ubingwa Ubingwa wa soka Tanzania bara.
Huku Azam ikitwaa Ubingwa wa soka Tanzania bara kwa mara ya kwanza, Timu nyingine kongwe ya Simba msimu huu imeyumba sana ambapo haina hata uhakika wa kushika hata nafasi ya tatu baada ya kudorora hasa kwenye mzunguko wa pili wa Ligi hii inayoshirikisha jumla ya timu 14 ambapo inashika nafasi nne ikiwa na pointi 37.
Katika Ligi ya Mwaka huu Timu ya Mbeya City iliyoleta changamoto kubwa katika mzunguko wa kwanza wa ligi,imeishia kunawa baada ya kudorora katika raundi ya pili na hivyo kuishia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 kwa sasa Huku timu zote zikiwa zimebakisha mechi moja moja.

clouds stream