Wednesday 2 April 2014

WANYAMA NA MAAJABU YAO.


KUSAFIRI KWA  MBAWAKAWA 
Mbawakawa hutumia kinyesi kwa ma- kusudi mbalimbali. Mdudu huyo hu- tumia kinyesi kama chakula na mahali pa
kutagia mayai. Wadudu fulani wa kiume huwapa wadudu wa kike kipande kiku- bwa ili kuwavutia. Wadudu hao hupigania kinyesi ambacho hakijakauka. Watafiti wa- lishuhudia mbawakawa 16,000 wakivamia rundo kubwa la kinyesi cha ndovu na kuki- maliza kwa muda wa saa mbili tu.
Aina fulani ya mbawakawa huviringisha kipande cha kinyesi kama mpira, halafu wanaondoka nacho na kukizika kwenye udongo laini. Mbawakawa huviringisha mpira huo kwa kufuata mstari ulionyooka, ili waondoke haraka na kuepuka kunya- ng’anywa na mbawakawa wengine.
Hata hivyo, mbawakawa huepukaje ku- zunguka mahali palepale, hasa usiku?

Fikiria hili: 
Mwanzoni utafiti ulionyesha kwamba mbawakawa wanasafiri kwa kute- gemea mwangaza wa jua au mwezi, hata
Je, wajua? Mbawakawa hulegeza na kuongeza rutuba kwenye udongo, husambaza mbegu
za mimea, na kudhibiti idadi ya nzi.

hivyo, wanaweza kusafiri kwenye mstari ulionyooka usiku usio na mwangaza wa mwezi. Watafiti nchini Afrika Kusini waligu- ndua kwamba mbawakawa husafiri si kwa kutazama nyota, bali kwa kutumia mwa- ngaza unaotoka kwenye kikundi cha nyo- ta cha Kilimia. Kulingana na gazeti Cur- rent Biology, huo ndio “uchunguzi wa kwanza unaoonyesha viumbe wanaotege- mea kundi la nyota la Kilimia katika kusa- firi.”
Mtafiti Marcus Byrne , anasema kwa- mba mbawakawa wana “mfumo bora unaowawezesha kuona usiku usio na mwangaza wa nyota, bila kutumia akili nyi- ngi.” Anaendelea kusema: “Hivyo basi, wanaweza kuwafundisha wanadamu kuta- zama na kuchanganua habari ngumu kue- leweka.” Kwa mfano, roboti inaweza kuwe- kewa programu ili ipekue vifusi vya jengo lililoporomoka kwa kuiga mfumo wa kusafi- ri wa mbawakawa.

Una maoni gani? 
Je, uwezo wa kusafiri wa mbawakawa ulijitokeza wenyewe? Au je, ni kazi ya ubuni? ̨ 

clouds stream