Friday, 11 April 2014

CNN YATANGAZA MOVIE ZA KIAFRIKA AMBAZO SIO ZA KUKOSA.

1. FROM A WHISPER (KUTOKA MNO'NGO,NO).

Filamu hii ni ya uweli na unaongelea matukio yaliyozunguka tukio la kulipuliwa kwa ubalozi wa Marekani huko Kenya mwaka 1998. Movie hii inasifika kua na mchanganyiko mzuri wa nyimbo na waigizaji wenye vipaji.

2. VIVA RIVA.

Filamu hii imeigizwa akimzunguka kijana aitwae Riva ambae ana kiu cha maendeleo na pia ni mtu wa vikundi. Katika mishe mishe zake Riva akapata taarifa juu ya dili za mafuta ya petroli na kutaka kutawala soko zima la uuzaji mafuta. lakini hakuwa mwenye kikundi pekee, hapo ndipo utata unapoaanza;.

3. SINKING SAND (MCHANGA UNAOZAMA).

Filamu hii inaongelea zaidi unyanayasaji wa kijinsia na gomvi za kindoa. Filamu hii inamuongelea jamaa ambae alipata ajali na kuharibika vibaya na baada ya hapo kua na chuki kubwa kwa mkewe pamoja na wivu wa hali ya juu.

4. MWANSA THE GREAT.

Filamu hii imetawaliwa na waigizaji watoto ambao wamefanya kazi nzuri na kufanya Afika iwake kwa kujulisha kua kizazi kijacho hakitakosa waigizaji wazuri. Filamu hii inamuelezea mtoto aitwae Mwansa akiwa na kazi kubwa ya kuonesha kua yeye bi kiongozi mzuri wa kiafrika.

5.MOLAADE.

Kuna jambo ambalo wanaume wengi na jamaa nyingi hua zinapata shida kuliongelea. Swala la ukeketaji. Filamu hii inaongelea hali halisi ya ukeketaji na madhara yake kwa njia ya maigizo ambapo hadithi yake ni ya kusisimua na pia kwa upande fulani kusikitisha.

6. WHITE WATERS

Filamu hii ni nzuri sana kwa jinsi ya kwamba inaamsha hisia ya kua unaweza kufanya chochote kizuri pasipokua na shaka kama utajiamini.n Filamu hii ianongelea hadithi ya kijana ambae ni mlemavu na jinsi alivyogundua kua ni mkimbiaji mzuri sana.

clouds stream