FIFA imeweka hadharani orodha ya wachezaji ambao wana kasi zaidi wakiwa uwanjani. Oorodha hii imetegemeana hasa na kasi ya juu zaidi aliyoionesha mchezaji katika mechi kadha ndani ya msimu wa 2012-2013. Hii ndio orodha ya watu hao wenye kasi zaidi uwanjani.
1. ANTONIO VALENCIA(MANCHESTER UNITED).
Mchezaji Antonia Valencia wa manchester united anaongoza kwa spidi kwenye msimu huu akiwa na rekodi ya spidi 35.2 km/hr.
2. GARETH BALE (REAL MADRID).
Mchezaji Gareth Bale anashkilia nafasi ya pili kwa kuandika spidi iliyorekodiwa ya 34.7 km/h ambapo mchezaji huyu wa bei ghali zaidi hutumia mbio zaidi katika uchezaji wake.
3. AARON LENON (TOTENHAM HOTSPURS).
Aaron Lenon ameandika spidi ya 33.8 km/h ambapo mchezaji huyu alishika nafasi ya kwanza msimu wa 2011-2012
4. CHRISTIANO RONALDO (REAL MADRID).
Mchezaji bora wa mwaka Christiano Ronaldo ameandika spidi ya 33.6 km/h.
5. THEO WALCOT (ARSENAL).
Mchezaji wa Arsenal Theo Walcot ameshikilia nafasi ya 3 kwa kua na spidi ya 32.7 km/h ambapo amemzidi mpaka lionel messi wa Barcelona kwa kutoka nduki.
6. LIONEL MESSI (BARCELONA).
Lionel Messi amekaa katika nafasi ya sita ambapo speed yake ya kurekodiwa ni 32.5 km/h
7. WAYNE ROONEY (MANCHESTER UNITED).
Wayne Rooney wa Man United ameandika rekodi ya kasi kua 32.1 Km/h ambapo pamoja na kasi hii, mchezaji huyu amekua na uwezo mkubwa wa kukaa na mpira pamoja na kutumia nguvu.
8. FRANCK RIBERY (BAYERN MUNICH).
Franck Ribery wa Bayern Munich na ufaransa ameshikilia nafasi ya 8 katika kufukuza upepo akiwa uwanjani kwa kuwa na kasi ya 30.7 km/h ambapo hajapishana na mwenzie Arjen Robben.
9. ARJEN ROBBEN (BAYERN MUNICH).
Kama alivyo Franck, ndivyo alivyo Robben kwa kasi ambapo pia amefikisha kasi ya 30.7 km/h. Akionekana kama mzee ila kwenye mbio, mchezaji huyu ni hatari sana kwa walinzi wa timu pinzani.
10. ALEXIS SANCHEZ (BARCELONA).
Alexis Sanchez amefikisha kasi ya 30.1 km/h ambapo amejumuika na wachezaji wengine wa ligi ya Hispania katika nafasi hio huku akionesha kiwango kizuri mbele ya goli.