Lowassa awashitukiza soko la Tandika
Mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza Juma Duni Haji katika soko la Tandale.
Aidha, wagombea hao waliwasili katika soko hilo asubuhi ya leo ambapo shughuli zilisimama kwa muda, kabla ya kuanza mazungumzo na wafanyabishara hao alikaribishwa chai na mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.
Ziara hiyo ya kushitukiza iliyoanzia Mbagala siku ya jana ni maalumu kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa hali ya chini kuhusiana na matatizo yanayowakumba katika maisha yao ya kila siku.