Serikali yapiga marufuku Mgombea urais kupanda daladala
Serikali kupitia jeshi la Polisi nchini Tanzania imepiga marufuku wagombea urais kupanda daladala ikiwa ni siku moja imepita tokea mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake Juma Duni Haji kupanda daladala.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Kamanda wa Kanda maalumu jijini Dar es salaam Suleiman Kova amesema jeshi la Polisi limepiga marufuku wagombea urais kupanda dala dala kufuatia wananchi wengi kuacha shughuli zao na kuelekea kwa wanasiasa hao suala linaloweza kuhatarisha usalama wao.
Katika hatua nyingine Lowassa alipanda dala dala jana katika maeneo ya Gongo la Mboto kuelekea Chanika kujionea shida mbalimbali za wananchi hao akiwa na mgombea Mwenza wake Juma Duni Haji suala lililopelekea wananchi kufurahi kuwaona wagombea hao katika eneo hilo ambalo wamedai hakuna kiongozi aliyewahi kufika tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961.