Wednesday, 26 August 2015

Waziri wa zamani Masha afikishwa Mahakamani

Waziri wa zamani Masha afikishwa Mahakamani

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Lawerence Masha(mwenye tisheti nyeusi) akishuka kwenye gari katika mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Lawrence Fortunatus Masha (katikati) akitolewa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, akishitakiwa kwa  kosa la kutumia lugha ya matusi na kejeli dhidi ya maafisa wa Polisi. 
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani Lawrence Fortunatus Masha 47, leo  ameafikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, akishitakiwa kwa kutumia lugha ya matusi na kejeli dhidi ya maafisa wa Polisi.
Akisoma mashita dhidi ya mshitakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Waliwandwe Lema, Mwendesha Mashitaka Wankyo Simon amesema mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 24 mwaka huu katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Upande wa Mashitaka umesema mshitakiwa alitumia lugha ya matusi na kejeli dhidi ya Inspekta Msaidizi Juma Mashaka na maafisa wengine wa polisi.
Kwa mujibu wa mashitaka, mshitakiwa alisema “Polisi ni washenzi waonevu hamna shukrani, huruma wala dini,” maneno ambayo yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mshitakiwa amekana mashitaka hayo na upande wa mashitaka umesema uchunguzi bado unaendelea.
Mshitakiwa amepelekwa mahabusu kwa kile kilichodaiwa kusubiriwa kwa uthibitisho wa hati za wadhamini.
Miongoni mwa masharti yaliyotolewa na mahakama ili kupata dhamana ni kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, watakaosaini dhamana ya shilingi milioni moja.
Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Septemba 7 mwaka huu.

clouds stream