Urais 2015: Zitto Kabwe azilipua CCM na UKAWA
Zitto Kabwe akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe leo amewalipua chama
cha Mapinduzi CCM pamoja na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuwa
hawana jipya katika kinyanganyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika oktoba 25,2015.
“Kama untaka siasa za Mbwembwe nenda CCM,Kama unataka siasa za ulaghai nenda UKAWA na kama unataka siasa za misingi siasa za issues ni ACT-Wazalendo” amesema Zitto Kabwe.
Amesema kwamba mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika kampeni zake anazungumzia hasa Barabara utadhani anakwenda kuwa Rais wa Barabara, wakati UKAWA wakiwa hawana jipya.
Chama chake kina ajenda nne ambazo
(i)Haki ya Watanzania kwenye hifadhi ya jamii kwa kupata bima afya,
(ii)Uchumi unaozalisha Ajira
(iii)Afya
(iv)Elimu