Azam Bingwa Kagame Cup 2015
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadick (wa pili kushoto)
akimkabidhi la ubingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati, Kagame baada ya
kuifunga Gor Mahia ya Kenya 2-0 leo uwanja wa Taifa jijini Dares
salaam.
Azam iliingia fainali baada ya kuitandika KCCA ya Uganda goli 1-0 huku Gor Mahi ya kenya ikiingia fainali baada ya kuitandika Khartoum ya Sudan magoli 3-1 katika michezo ya nusu fainali.
John Bocco (Adebayor) alikuwa wa kwanza kuipatia Azam bao la kwanza akiunganisha krosi ya Kipre Cheche katika dakika ya 16 ya mchezo katika kipindi cha kwanza baada ya safu ya ulinzi ya Gor mahia inayoongozwa na Haruna Shakava kupotena na kumpa Bocco nafasi ya kufumania Nyavu.
Katika kipindi cha kwanza Bocco na Kipre walikosa magoli katika dakika tofauti huku kwa upande wa Gor Mahia Michae Olunga na Erick Ochieng wakipata wakati mgumu baada ya beki wa Azam Paschal Wawa kuonyesha kuwamudu wachezaji wote hao wa Gor Mahia na mpaka mapumziko Azam walikuwa mbele kwa Goli moja.
Katika kipindi cha pili Aucho Khalid wa Gor Mahia alionekana kuichezesha timu hiyo huku akitoa pasi nyingi za pembeni zilizokuwa zikimkuta Erick Ochieng lakini jitihada zake azikuzaa matunda na Aucho Khalid alimchezea madhambi Kipre Cheche katika eneo la hatari madhambi yalioyozaa goli katika dakika ya 64 ya mchezo katika kipindi cha pili.
Mpaka dakika ya 90 Azam waliibuka washindi wa Michuano hiyo wakiwachapa Gor Mahia ya Kenya Magoli 2-0 katika mchezo wa fainali.