Mgomo wa Walimu watikisa Kenya, Kenyatta atoa kauli

Mgomo wa Walimu nchini Kenya.
Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za umma na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT amesema kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka kwa serikali.
Amesema chama hicho kilikuwa kimeishauri serikali ifunge shule “zamani”. Mahakama inatarajiwa kuamua Ijumaa ijayo iwapo mgomo huo wa walimu, ambao umesitisha masomo muhula wa tatu, ni halali au la.