UKAWA: Mabadiliko mkoani Tabora
Mgombea Urais wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa amepata mapokezi makubwa mkoani Tabora
alipowasili na kuwahutubia wananchi wa Mji wa Tabora.
Katika mkutano huo Lowassa alitumia fulsa hiyo kuinadi sera za umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA itakayotumika kwa miaka mitano ijayo ikiwa atafanikiwa kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25, oktoba mwaka 2015.