Thursday, 3 September 2015

Tundu Lissu,Gwajima wafunguka kuhusu Dr. Slaa

Tundu Lissu,Gwajima wafunguka kuhusu Dr. Slaa



Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu.
Kufuatia Katibu Mkuu Chadema Dr.Wilbrod Slaa kutangaza kujivua uanachama wa Chadema na kustaafu siasa huku akimshushia tuhuma  mgombea urais wa chama hicho Edward Lowassa,hatimaye Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu pamoja na Mchungaji Josephat Gwajima wamefunguka.
Kwa mujibu wa Tundu Lissu kupitia   moja ya Redio  nchini  alipinga maelezo yaliyotolewa na Dk. Slaa na kudai kuwa yeye ndiye wa kwanza kutoa wazo la kumkaribisha Lowassa  kwenye chama hicho.
“Kamati kuu ilimpitisha mwezi January ikathibitisha tena mwezi April, ilipofika mwezi wa Tano ni Dk Slaa ndiye aliyeanzisha tena mazungumzo ya kumleta Lowassa ndani ya Chadema,” alisema.
“Yeye anasema Gwajima alikuwa mshenga, hajasema mposaji ni nani, nani aliyemuendelea Gwajima kumwambia kwamba tunamtaka Lowassa, sio mwingine ni huyo Dk. Slaa,” alisisitiza.
Lissu amedai  kuwa chanzo cha Dk. Slaa kugeuka mpango aliokuwa akiusuka yeye ni mtazamo tofauti alioupata kwa mkewe Josephine ambaye alizua ugomvi mkubwa.
Kilichoharibika ni first lady, mama alikataa,” alisema na kufafanua kuwa siku ambayo Kamati Kuu ya Chadema ilimpokea Edward Lowassa katika chama hicho mkewe Josephine alimtupia mabegi nje na kusababisha alale ndani ya gari.
Kwa upande wa  Askofu Josephat Gwajima amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa kuwa alishiriki kama ‘mshenga’ kumshawishi  Edward Lowassa kuhamia Chadema
Katika maelezo yake  Dk. Slaa alimtaja Askofu Gwajima kama mshenga na ndiye   alimshawishi ampokee Lowassa huku akidai kuwa askofu huyo alimtamkia kuwa maaskofu 30 walihongwa na  Lowassa.
Aidha, Askofu Gwajima amesema Dk. Slaa ni muongo mkubwa akidai kuwa  ameamua kuwashambulia maaskofu hao kwa kuwa anafahamu hawana majukwaa ya kumjibu kama ilivyo kwa wanasiasa.
Gwajima alidai kuwa yeye aliitwa kama msuluhishi ndani ya Chadema na sio mshenga wa kumleta Edward Lowassa.
Katika hatua nyingine  Gwajima ameliambia moja ya gezeti kubwa hapa nchini Dk. Slaa ametumwa na watu anaowafanyia kazi.

clouds stream