Thursday, 3 September 2015

Mbatia amvaa Slaa, awaangukia Maaskofu

Mbatia amvaa Slaa, awaangukia Maaskofu


Mwenyekiti Mwenza UKAWA James Mbatia.
Mwenyekiti mwenza wa UKAWA James Mbatia amejibu tuhuma zilizotolewa na Dkt Slaa dhidi ya Mgombea Urais wake Edward Lowassa huku akiwataka maaskofu kumsamehe Dkt. Slaa kwa yale aliyoyasema wakati akitangaza kujiuzulu Chadema na kustaafu siasa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kujibu baadhi ya mambo aliyosema Dkt. Slaa Mbatia amewaomba  Watanzania waelewe UKAWA inasimamia utu, uzalendo, uadilifu, umoja, uwazi, uwajibikaji ndani ya Tanzania.
Amesema kuwa hoja alizo zitoa Dkt. Slaa zina ashiria kwamba CCM wameshindwa hoja, mara kuleta mambo ya udini, mara wanaibua hili mara lile.
Amesema wagombea wao wa  urais walikaa na Dokta Slaa alisema yeye   ni bora kuliko wote, leo hii anasema hajawahi kutia nia, kweli? Eti Lowassa akija ndani ya Ukawa atakuja na Wenyeviti wa CCM   kitu  ambacho  hakuwahi kusema.
Lowassa hajawahi kutamka kuwa akija ndani ya UKAWA atakuja na wabunge 50, wenyeviti wa CCM na Makatibu mbalimbali wa mikoa.
Amehoji kuwa kama  Dkt. Slaa ni muadilifu alipewa Milioni 500 mwaka 2008 anakuja kusema leo baada ya miaka 7 , suala la rushwa zaidi ya miaka 7 usiripoti halafu uje useme leo, kusema uongo ni kazi sana.
“ Tuibue masuala yote na kashifa za kuuzwa kwa nyumba, kuna mtu atabaki salama? Amesema Mbatia
Amesema  kuwa Wanasiasa hasa wale wa CCM Mwakyembe na Sita, wanaotaka midahalo waje waongee na yeye  wasimsumbue Mgombea wao, Lowassa sio saizi yao.
Ametumia fulsa hiyo  kuwaomba watanzania wote ambao ni zaidi ya milioni 46, wasiruhusu nchi yao ikaharibiwa na watu 100. Watu wachache wanaotaka eti kwa lolote lile lazima waendelee kubaki madarakani, wanasema hapana.
Kwa upande wa tuhuma dhidi ya viongozi wa dini Mbatia amesema kilichowasikitisha ni yeye kuhusisha watu wengine wasiohusika kwenye jamii yetu  ambao ni viongozi wa dini wakiwemo maaskofu.
Amevitaka vyama vya siasa  viachiwe  visuguane  vyenyewe  huku akiwa omba Viongozi wa dini walio onewa kwa kauli ya Dkt. Slaa, wasamehe na waachane nayo.
Hotuba ya Dkt.Slaa alipotangaza kujiuzulu siasa na Kumvaa Edward Lowassa. Angalia hapa kupitia Sasa TV

clouds stream