Friday, 13 May 2016

Besigye Ajiapisha Urais Uganda, Akamatwa Na Polisi

Besigye Ajiapisha Urais Uganda, Akamatwa Na Polisi

Tarehe May 12, 2016ddd
ddd
Dkt Kiiza Besyige
Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi  vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wanachama wa chama chake na kula kiapo cha urais wa taifa hilo.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana akila kiapo mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya jaji wa mahakama ya juu.
Video hiyo ilisambazwa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.
Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.

clouds stream