Thursday 26 May 2016

Tozo Daraja La Nyerere Kupitiwa Upya

Tozo Daraja La Nyerere Kupitiwa Upya

Tarehe May 26, 2016
746a05242f0e65acccb45c83318ae029
Kufuatia malalamiko ya watumiaji wa daraja la Nyerere lililopo Kigamboni, serikali inatarajia kufanya mapitio ya viwango vya tozo zinazotumika kwa vyombo vya usafiri vinavyopita kwenye daraja hilo.
Akizungumza na gazeti la serikali la kila siku, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (anayeshughulikia Ujenzi), Joseph Nyamhanga, alisema tangu waanze makusanyo, wamepokea ushauri na maoni na kisha watafanya mapitio ya viwango.
“Kwa sasa bado ni mapema sana, hatuna hata mwezi mmoja toka tuanze kupokea tozo, tunaendelea kupokea ushauri na baada ya mwezi mmoja tutakaa na kufanya mapitio tena kuangalia viwango hivyo,” alisema Nyamhanga.
Aidha alisema Wizara pia itaangalia namna ya kuweka mfumo ambao utawanufaisha zaidi watumiaji wa daraja hilo wa mara kwa mara kuwezesha kuwapo utaratibu wa kulipia tiketi za msimu zitakazotoa nafuu.
“Ushauri wangu kwa wananchi wanaotumia daraja hilo ni kwamba wavute subira wakati tunaangalia hali ikoje, lakini waelewe duniani kote barabara za kulipia na hata madaraja yapo, hii ni mfumo ambao upo duniani kote,” alifafanua.

clouds stream