Rais Wa Brazil Dilma Rousseff Atumbuliwa
Tarehe May 12, 2016
Hatimaye, Bunge la Seneti Brazil limepiga kura kuamua kuidhinisha kura ya kutokuwa na imani dhidi ya kiongozi wa taifa hilo Dilma Rousseff.
Kutokana na kura hiyo Rais Dilma atasimamishwa kazi ya urais kwa siku zisizozidi 180 wakati bunge hilo la Seneti litakagua tuhuma zinazomkabili.
Bi Rousseff anatuhumiwa kubadili kinyume cha sheria fedha za serikali kuficha nakisi inayoongezeka ya umma kufuatia kuchaguliwa kwake tena mnamo 2014, tuhuma ambazo amezikana.
Maseneta 55 waliunga kuidhinishwa kura hiyo ya kutokuwab na imani dhidi ya 22 bungeni katika kikao cha zaidi ya saa 20.
Kufuatia kusimamishwa kwa Rais huyo Makamu wa rais Michel Temer atashikilia madaraka wakati kesi dhidi ya Bi Rousseff inaendelea.