Tuesday, 2 June 2015

Meli yazama nchini China, abiria 400 hawajulikani walipo

Meli yazama nchini China, abiria 400 hawajulikani walipo

Tarehe June 2, 2015
Vikosi vya uokoaji tayari vikielekea eneo la tukio.
Vikosi vya uokoaji tayari vikielekea eneo la tukio.
Boti za kijeshi kwa ajili ya kutoa msaada.
Boti za kijeshi kwa ajili ya kutoa msaada.
Meli ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imezama baada ya kukumbwa na upepo mkali katika Mto Yangtze kusini mwa  nchi ya China.
Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua watu wanane wameokolewa mpaka sasa na kazi inaendelea ya kuwaokoa abiria wengine.
Waziri Mkuu Li Keqiang anaelekea katika eneo la tukio hivisasa kuangalia namna ya kuwaokoa abiria waliokuwa wanasafiri katika meli hiyo huku  kazi ya uokoaji imekwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa. Meli hiyo ilizama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mashariki mwa mji wa Nanjing kwenda Chongqing kusini magharibi ilipozama. Meli hiyo, Dongfangzhixing au Nyota ya Mashariki ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa shirika la usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.
Nahodha na mhandisi mkuu, ambao ni miongoni mwa waliokolewa wamekaririwa wakisema kuwa meli ilikumbwa na kimbunga na kuzama haraka. Waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Shanghai.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.

Prof. Muhongo, Ngeleja, Kamani kutangaza nia leo

Prof. Muhongo, Ngeleja, Kamani kutangaza nia leo

Tarehe June 2, 2015
Prof.Sospeter  Muhongo,Williaum Ngeleja,  Dk. Titus Kamani  nao wanatarajia kutangaz nia kugombea urais leo.
Prof.Sospeter Muhongo,Williaum Ngeleja, Dk. Titus Kamani nao wanatarajia kutangaz nia kugombea urais leo.
Mbio za urais kupitia kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi imezidi kushika kasi huku Wanasiasa  mbalimbali  kutoka chama cha Mapinduzi wakijitokeza kutangaza nia pamoja na kuweka vipaumbele vyao endepo watachaguliwa kuwakilisha   chama chao kuiongoza nchi.
Aidha, wanasiasa wanaotarajia kutangaza nia leo ni Mbunge wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja pamoja, Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani  na  aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na chama cha Mapinduzi CCM imebainisha kuwa wanasiasa wanaotaka kuwania urais watachukua fomu makao makuu ya chama hicho yaliyopo mkoani Dodoma ifikapo juni 3 siku ya jumatano wiki hii.

Urais 2015: Makongoro Nyerere atangaza kuwang’oa mafisadi Tarehe June 2, 2015

Urais 2015: Makongoro Nyerere atangaza kuwang’oa mafisadi

Tarehe June 2, 2015
Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere akitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM, katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama jana.
Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere akitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM, katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama jana.
Makongoro Nyerere akivishwa na wazee mgolole baada ya kutangaza nia ya nia ya kugombea urais kupitia CCM.
Makongoro Nyerere akivishwa na wazee mgolole baada ya kutangaza nia ya nia ya kugombea urais kupitia CCM.
Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere naye ametangaza nia    ya kuwania urais kijijini kwao Mwitongo wilayani Butiama jana.
Akizungumza na Wananchi Makongoro, amesema anatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo kutokana na kukerwa sana na rushwa, kwa kuwa  inasababisha Watanzania wengi kupoteza haki zao.
Pia Makongoro amesema anatambua kuwa kuna makundi ndani ya CCM. Akipata   nafasi ya urais na baadaye  kuwa mwenyekiti wa CCM atayamaliza na wote tutabaki kitu kimoja.
Amesisitiza kuwa ataboresha hali ya majeshi ya Tanzania, pamoja na wanafunzi elimu ya juu kupata mikopo kwa wakati.
Amesisitiza kuwa Rais Kikwete, amefanya kazi nzuri katika kipindi cha uongozi wake, lakini kuna watu wanamhujumu ili aonekane hafanyi kazi.
Makongoro anakuwa mwanasiasa wa tano kutangaza nia ya kutaka kuwania urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, wengine ni Luanga Mpina,Edward Lowassa, Steven Wassira, Mwigulu Nchemba, Lazaro Nyalandu huku wengine wakijitokeza tena leo.

clouds stream