Tuesday, 2 February 2016

Muuaji Kigogo Wa CUF Atoboa Siri Ya Aliyemtuma

Muuaji Kigogo Wa CUF Atoboa Siri Ya Aliyemtuma

Tarehe February 2, 2016
Simon Shilage kijana anayedaiwa kumuua Diwani wa CUF.
Simon Shilage kijana anayedaiwa kumuua Diwani wa CUF.
Kijana mmoja aliyefahamika kwaji  na la Simon Shilage miaka 22 amekamatwa   na jeshi   la Polisi akidaiwa  kushirikiana na mwenzake kumuua Diwani wa kata ya Kimwai huko Muleba Ndg. Faustine Muliga wa chama cha wananchi CUF.
Kwa mujibu wa Chanzo chetu kutoka Muleba kimebainisha kuwa kijana huyo alikamatwa jioni ya jana na wananchi wa kijiji cha Kyota akijaribu kutoroka akiwa na  panga lenye damu alilotumia kumuua diwani Muliga.
Alipohojiwa kwa nini ametekeleza mauaji hao   Simon amekiri kuwa kweli yeye na mwenzie mmoja (hakumtaja jina) ndio waliomuua Mhe. Muliga kwa kumkata mapanga akiwa nyumbani kwake wakati  ana angalia taarifa ya Habari.
Kijana huyo amesema kazi hiyo  ya mauaji  hayo walitumwa na aliyekua mgombea udiwani wa Kata hiyo kwa tiketi ya CCM kwenye uchaguzi uliopita, ambaye alikua mpinzani wa Muliga lakini alishindwa kwenye uchaguzi.
Ameongeza kuwa Mgombea huyo aliwaahidi kiasi cha shilingi milioni 1.5 ikiwa watafanikiwa kumuua Muliga na aliwapa “advance” ya shilingi laki moja na nusu (150,000/=).
Baada ya makubaliano hayo vijana hao walimvamia Muliga nyumbani kwake majira ya saa 2 usiku akiangalia “Taarifa ya Habari” ambapo walimkata mapanga maeneo mbalimbali mwilini mwake kabla ya kutokomea kusikojulikana.
Imeelezwa kuwa Simoni  alikamatwa na wananchi wenye hasira kali ambao walitaka kumuua ambapo wali mkata sikio  na kisha  akaokolewa na Polisi.
Mtuhumiwa  huyo   anashikiliwa kituo cha Polisi Muleba kwa upelelezi, kabla ya kupandishwa Mahakamani kujibu tuhuma za Mauaji.
Mtandao huu umemtafuta aliyekuwa mgombea udiwani anayedaiwa  kuwatuma vijana hao bila mafanikio.
Diwani wa Kimwani, Kagera, Faustine Muliga (CUF) aliyeuawa.
Diwani wa Kimwani,  Faustine Muliga (CUF) aliyeuawa.

TFF Yampongeza Kikwete Kukubali Uteuzi Wa CAF

TFF Yampongeza Kikwete Kukubali Uteuzi Wa CAF

Tarehe February 2, 2016
Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Rais  Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete kwa kukubali uteuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) na GAVI utakaomfanya kuwa bingwa wa chanjo na balozi wa mradi wa Africa United Duniani.
“Familia ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa chanjo na hasa katika maendeleo ya vipaji na wanamichezo kwa ujumla na namna chanjo inavyoweza kuwapa watoto siyo tu fursa ya maendeleo bali haki ya kuishi kukua” amesema Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Katika barua hiyo kwa Rais Mstaafu Kikwete, Malinzi ameelezea furaha ya TFF kuona kiongozi wa Tanzania akiongoza mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi cha sasa na kijacho katika Afrika na dunia kwa ujumla.
“TFF itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na ushirika wa chanjo” ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou.

Guardiola Amtaka Pogba

Guardiola Amtaka Pogba

Tarehe February 2, 2016
Guardiola
Guardiola
Pep Guardiola hana hata siku moja katika kibarua chake kipya huko jijini Manchester akikinoa kikosi cha Man City kwa mda wa miaka minne lakini ameanza kwa kasi ya ajabu baada ya kumtaka kiungo wa Juventus Paul Pogba.
Guardiola anatarajia kaunza kazi katika kipindi cha majira ya joto lakini anataka kumsajili kiungo huyo kwa pauni milioni 80 n.
Guardiola ameutaka uongozi wa Man City kufanya kila wawezalo kuhakikisha kiungo huyo anatua uingereza.
Paul Pogba
Paul Pogba

clouds stream