Thursday, 1 September 2016

Tanzania Daima Wafurumushwa Kisa Deni La Mbowe.

Tarehe September 1, 2016 9/1/2016
image
Tanzania Daima Wafurumushwa Kisa Deni La Mbowe ­ Tanzania ­ Habari/News | Hivisasa Blog http://hivisasa.co.tz/habari/tanzania­daima­wafurumushwa­kisa­deni­la­mbowe 2/10 Madalali wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wamefika katika ofisi za gazeti la Tanzania Daima asubuhi hii na kuanza kutoa vifaa ofisini kutokana na deni la pango la mmiliki wa gazeti hilo, Freeman Mbowe.
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena amesema kuwa wako katika pilikapilika za kuhakikisha kuwa uzalishaji wa gazeti unafanyika kama kawaida licha ya kadhia hiyo.
Hivi karibuni NHC ilitoa orodha ya wadaiwa sugu wa kodi akiwemo pia Freeman Mbowe ambapo lilisema kuwa litawatoa kwa nguvu wadaiwa sugu hao kutoka katika nyumba hizo.
Ofisi za gazeti hilo zipo katika jengo moja na ilipo Klabu maarufu ya Billicanas ambayo pia inamilikiwa na Mbowe.image (1)image (2)

Mkapa Ataka Mageuzi Makubwa Sekta Ya Uwekezaji

Tarehe September 1, 2016
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa.V 1
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, amezitaka nchi za Africa Mashariki kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya uwekezaji ili kuweza kuleta maendeleo barani humu.

Mkapa amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya Taasisi ya Mazingira ya Uwekezaji Afrika (ICF), ya kusherehekea miradi ipatayo 73 ya mageuzi ambayo imelenga kuifanya Afrika kuwa sehemu bora ya kufanyia biashara.

Mkapa ambaye pia ni Mwenyekiti Mweza wa Bodi ya ICF, iliyoudwa kwa lengo la kuthibitisha uwepo wa mageuzi ya haraka katika sekta ya uwekezaji ameshauri matumizi ya fedha kidogo kidogo kwa lengo la kuleta matokeo makubwa katika sekta binafsi, serikali pamoja na nchi kwa ujumla.

“Imefikia kipindi kwa nchi za Afrika kufuata mfumo huu wa ICF ili kuweza kuleta mageuzi makubwa ya uwekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo za kiserikali pamoja na binafsi na uwepo wa ongezeko la wajasiriamali, ” amesema Mkapa.

 Amesema miradi mingi iliyoweza kutekelezwa kati mwaka 2007 na 2016 imesaidia kusajiliwa kwa miradi mingine mingi, kulipa kodi zao kwa urahisi, kupitisha mizigo kwa mfumo wa forodha kwa haraka na urahisi pamoja na kusuluhisha migogoro ya kibiashara.

Mkapa amesema, mfumo wa ICF umeweza kufanya kazi barani Afrika katika nchi zipatazo 21, kuweka mfumo mmoja wa kielektroniki kwa lengo la kurahisisha uondoshwaji wa mizigo na kuweka mifumo ya mtandao ya ulipaji kodi.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya ICF, Neville Isdell ameyataja maeneo maalum ya mafanikio, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa mahakama tisa za kibiashara na nne za usuluhishi kwa lengo la kusuluhisha migogo ya kibiashara kwa haraka na uwazi.

Isdell amesema, mfumo wa ICF umeweza kusaidia badhi ya nchi kuweza kuwa na mfumo wa kielektroniki wa uuzaji wa bidhaa, kukuza uwezo wa serikali kushirikiana na sekta binafsi kwa kupitia mpango wa ushirikiano kati ya sekta za umma na sekta binafsi.

Wananchi Wachoma Moto Jengo La Bunge Kupinga Matokeo Ya Uchaguzi

Tarehe September 1, 2016
Rais Bongo aliyeshinda muhula wa pili amekuwa madarakani tangu mwaka 2009
Rais Bongo aliyeshinda muhula wa pili amekuwa madarakani tangu mwaka 2009

Wananchi wenye hasira kali nchini Gabon wameliteketeza jengo la Bunge la nchi hiyo kwa moto baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa kuwa mshindi kwa asilimia 49.85.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Gabon, Pacome Moubelet Bouleya alisema kuwa Bongo amepata asilimia 49.80 katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi, akimshinda mpinzani wake Jean Ping aliyepata asilimia 48.23 ya kura zote.

Bongo anadaiwa kupata kura 5,594 ya idadi ya watu 627,805 ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura. Bongo, 57, sasa ameshinda muhula wake wa pili kama kiongozi wa Taifa hilo dogo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, ambalo awali lilitawaliwa na baba yake kwa muda wa miaka 41.

Mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, vurugu ziliibuka zikiambatana na maandamano yaliyopelekea kuchomwa moto kwa jengo hilo la bunge.gabon-83592b8f4997478e57f7151d4462ca3d9acc27895gabon005jpg.jpg.size.custom.crop.1086x72414102666_1211152902282035_5678415901271255371_n

clouds stream