Tarehe September 1, 2016
Rais Bongo aliyeshinda muhula wa pili amekuwa madarakani tangu mwaka 2009
Wananchi wenye hasira kali nchini Gabon wameliteketeza jengo la Bunge la nchi hiyo kwa moto baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa kuwa mshindi kwa asilimia 49.85.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Gabon, Pacome Moubelet Bouleya alisema kuwa Bongo amepata asilimia 49.80 katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumamosi, akimshinda mpinzani wake Jean Ping aliyepata asilimia 48.23 ya kura zote.
Bongo anadaiwa kupata kura 5,594 ya idadi ya watu 627,805 ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura. Bongo, 57, sasa ameshinda muhula wake wa pili kama kiongozi wa Taifa hilo dogo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, ambalo awali lilitawaliwa na baba yake kwa muda wa miaka 41.
Mara tu baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, vurugu ziliibuka zikiambatana na maandamano yaliyopelekea kuchomwa moto kwa jengo hilo la bunge.