Tuesday, 4 October 2016

RC: Watoto Wa Mitaani Wachapwe Viboko

Tarehe October 4, 2016
download-2V 1

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amefunguka na kuamuru watoto wa kiume wenye umri mkubwa wanaoishi mitaani mjini Sumbawanga, wacharazwe viboko mahakamani ili warudi na kuishi na familia zao.

Mkuu wa mkoa huo Zelothe Steven ameamuru wazazi na walezi wa watoto hao, wasakwe popote walipo na washtakiwe kwa kuwatelekeza watoto wao na kusababisha waishi mitaani.

Zelothe alitoa maagizo hayo katika Kikao cha 30 cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Rukwa (RCC), akiunga mkono ushauri alioutoa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Halfani Haule.

“Hii sasa imekuwa ni kero kubwa, zipo taarifa kuwa watoto hao wana wazazi wao lakini bado wanaonekana kukizurura mitaani na kuomba omba,” amesema Zelothe.

Watoto hawa sasa wamekuwa watukutu mitaani, kwa wale wenye umri mkubwa wasakwe , wakamatwe wafikishwe mahakamani na wapewe adhabu ya kucharazwa viboko kisha warejeshwe kwa wazazi wao.

“Kwa wazazi wenye watoto hawa nao wasakwe , wakamatwe na kufikishwa mahakamani ili iwe fundisho kwa wazazi wenye tabia isiyokubalika ya kuwatelekeza watoto wao na kusababisha waishi mitaani mjini hapa,” amesema Zelothe.

Naye, Dk Haule alishauri kuwa watoto 16 wanaoishi mitaani mjini humo, ambao wana umri mkubwa waliokamatwa hivi karibuni katika msako, waadhibiwe kwa kucharazwa viboko mahakamani kisha warejeshwe kwenye familia zao.

“jumla ya watoto 231 wote wavulana wamebainika kuwa wanaishi mitaani katika Mji wa Sumbawanga na umri tofauti katika msako wa hivi karibuni uliofanyika mjini hapa watoto 40 wamekamatwa na kupelekwa kuishi kwenye nyumba ya malezi ya Bethania, inayolea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Katika msako huo walikamatwa watoto 16 ambao wao wana umri mkubwa nashauri wacharazwe viboko mahakamani ili waweze kurudi kwenye familia zao.

Sunday, 2 October 2016

Kijembe Cha Zitto Kwa Mbowe Kufuatia Goli La ‘Mkono’ La Tambwe

Tarehe October 2, 2016
14-1V 1
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT­Wazalendo, Zitto Kabwe ametumia akaunti yake ya Twitter kutoa ujumbe wa utani kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe kuhusiana na goli la Amissi Tambwe alilofunga jana katika mechi ya watani wa jadi linalodaiwa kuwa ni goli la mkono.
Zitto ambaye pia ni mshabiki wa Simba ameandika ujumbe huo baada ya mechi hiyo kuisha ambapo timu hizo zilitoka sare ya goli 1­-1, akimkebehi Mbowe ambaye pia ni mshabiki wa Yanga.
Zitto aliandika maneno yafuatayo, “Mwenyekiti wangu Freeman Aikaeli Mbowe anatambua goli la mkono la Tambwe lakini hamtambui Lipumba.”
sad

Saturday, 1 October 2016

Mr Na Miss HIV Wapatikana

Tarehe October 2, 2016
ctqlmkexgaax6tsV 1
Mashindano ya kumtafuta kijana mtanashati (Mr) na Mrembo (Miss) waishio na virusi vya ukimwi (VVU) yamefanyika nchini Uganda na washindi kupatikana.
Nchini Uganda warembo wanaoishi na virusi vya ukimwi {VVU} wanashiriki mashindano ya kumpata malkia wa taji la warembo hao huku lengo likiwa ni kuondoa unyanyapaa dhidi ya watu wenye VVU.
Katika hatua za awali lilipotangazwa shindano hilo inasemekana takribani watu 150 walijitokeza wakitaka kushiriki katika shindano hilo.
Mashindano hayo pia yalihusisha watu wenye vipaji mbalimbali sio uzuri peke yake.
Inasemekana Uganda ni kati ya nchi zenye watu wengi wanaoishi na virusi vya UKIMWI, kwa takwimu za hivi karibuni zinasema mtu mmoja kati ya 14 ana maambukizi ya UKIMWI.ctqlmkexgaax6ts

clouds stream