Sunday, 1 January 2017

ARSENAL YAIBOMOA CRYSTAL PALACE 2-0, GIROUD AKIMJIBU MKHITARYAN SCORPION KICK

img-20161130-wa0008

Arsenal (4-2-3-1): Cech 6.5; Bellerin 7, Gabriel 6, Koscielny 6.5, Monreal 5; Elneny 6.5 (Coquelin 72, 6), Xhaka, 6; Perez 6 (Ramsey 72, 6), Iwobi 8 (Oxlade-Chamberlain 77), Sanchez 7; Giroud 7.5
Substitutes not used: Ospina (GK); Mustafi, Reine-Adelaide, Maitland-Niles
Manager: Arsene Wenger 6.5 
Scorers: Giroud 17; Iwobi 56
Booked: Monreal


Crystal Palace (4-2-3-1): Hennessey 7; Kelly 5, Tomkins 5, Dann 6, Ward 6; Flamini 5, Cabaye 5 (Mutch 65, 5); Townsend 6.5 (Lee 71, 5), Puncheon 5, Zaha 5; Benteke 6.5 (Campbell 77)
Substitutes not used: Speroni (GK); Sako, Husin, Phillips
Manager: Sam Allardyce 6 
Booked: Tomkins
Referee: Andre Marriner (West Midlands) 6
Attendance: 59,975 




Waziri wa mazingira auawa Burundi

Waziri wa mazingira amepigwa risasi na kufariki nchini BurundiWaziri wa mazingira amepigwa risasi na kufariki nchini Burundi
img-20161130-wa0008

Waziri wa mazingira huko Burundi Emmanuel Niyonkuru, amefariki baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.

Police wanasema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero .

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.

Rais wa Burundi PIerre Nkurunziza amesema kuwa waliohusika watachukuliwa sheria kali.

Waziri wa mazingira nchini Burundi Emmanuel NiyonkuruWaziri wa mazingira nchini Burundi Emmanuel Niyonkuru

Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi wameuawa tangu rais PIerre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu 2015, hatua ambayo wapinzani wanasema ni kinyume na sheria.

Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa serikali kuuawa.

Kwa miezi kadhaa taifa hilo limekuwa tulivu.

Korea Kaskazini kutengeza kombora la masafa marefu

Rais KIm Jong Un wa Korea Kaskazini

Rais KIm Jong Un wa Korea Kaskazini
img-20161130-wa0008

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa taifa lake linakaribia awamu ya kutengeza kombora la masafara marefu ambalo lina uwezo wa kubeba bomu la nuklia.

Katika hotuba ya kuukaribisha mwaka mpya iliopeperushwa hewani katika runinga ya taifa Bw Kim amesema kuwa Korea Kaskazini imeimarika kama taifa lenye uwezo wa kinyuklia mwaka 2016.

Pyongyang imefanya majaribio mawili ya kombora la kinyuklia katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ikiwa ni mojawapo ya majaribio yake makubwa kufikia sasa.

Hatua hiyo ilizua shutuma mbalimbali na kuvutia vikwazo vya kimataifa .

Haijulikani taifa hilo imekaribia kivipi kutengeza kombora la Kinyuklia ambalo linaweza kurushwa na kufika Marekani.

clouds stream