Waziri wa mazingira auawa Burundi
Waziri wa mazingira amepigwa risasi na kufariki nchini Burundi
Waziri wa mazingira huko Burundi Emmanuel Niyonkuru, amefariki baada ya kupigwa risasi mjini Bujumbura saa chache tu baada ya kuingia mwaka mpya.
Police wanasema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero .
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.
Rais wa Burundi PIerre Nkurunziza amesema kuwa waliohusika watachukuliwa sheria kali.
Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi wameuawa tangu rais PIerre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu 2015, hatua ambayo wapinzani wanasema ni kinyume na sheria.
Lakini hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa serikali kuuawa.
Kwa miezi kadhaa taifa hilo limekuwa tulivu.