Sunday, 3 May 2015

Urais 2015: Mrema apingana na UKAWA

Urais 2015: Mrema apingana na UKAWA


Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema ameibuka na kuwapingana na kauli ya UKAWA dhidi ya kuhisi kuahirishwa uchaguzi mkuu kutokana na kutokamilika kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha,Mrema amesema  hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa kuongoza nchi kwa muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Katika mkutano wa UKAWA wiki iliyopita walidai kuwa Serikali na Tume ya Uchaguzi (NEC) inachelewesha uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura kwa lengo la kutaka kumwongezea Rais Kikwete muda wa kukaa Ikulu.
Mrema amebainisha kuwa yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutoa wazo la kutaka Rais Kikwete aongezewe muda zaidi wa kukaa Ikulu kwa kuwa kuna mambo mengi ambayo ni ya muhimu kwa Taifa yanayotakiwa kukamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu.
Mrema amesema alitoa maoni hayo mwaka jana wakati viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) walipokutana na Rais Kikwete mjini Dodoma, lakini alishangaa kuona viongozi wengine wakipinga wazo hilo.

Urais 2015: Kamati kuu CHADEMA yajichimbia jijini Dar es salaam

Urais 2015: Kamati kuu CHADEMA yajichimbia jijini Dar es salaam



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa.
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA   chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, inatarajia   kujichimbia   jijini Dar es samaa  kuanzia  Mei 3-4 kujadili uchaguzi mkuu wa rais na wabunge unaotarajia kufanyika wiki ya mwisho ya mwezi oktoba.
Kwa  mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa CHADEMA  Tumaini Makene  imebanisha kwamba katika kikao hicho cha siku mbili, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;
  1. Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
  2. Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda
    dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
  3. Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.
  4. Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.
  5. Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Hata hivyo, hivi karibuni chama hicho kupitia umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA wameitaka tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kutoa ratiba nzima ya uchaguzi mkuu kwa mwaka  huu 2015.

Islamic state tena, yaua raia 300 nchini Iraq

Islamic state tena, yaua raia 300 nchini Iraq


Wanamgambo wa Islamic State.
Wanamgambo wa Islamic State.
Msemaji wa Serikali  nchini Iraq amesema kuwa wanamgambo wa islamic state wamewaua mamia ya watu wa yazidi waliokuwa wakiwazuilia eneo lililo kaskazini mwa nchi.
Aidha, Makamu wa rais nchini Iraq Osama al-Nujifi ameyalaani mauaji hayo akiyataja kuwa ya kikatili Taarifa zilisema kuwa hadi watu 300 waliuawa kwenye wilaya moja iliyo magharibi mwa mji wa Mosul siku ya ijumaa.
Wanamgambo wa islamic state wanadaiwa kudhibiiti   maeneo yaliyo kaskazini mwa Iraq kwa karibu mwaka mmoja uliopita ambapo waliwaua na kuwashika mateka maelfu ya watu wa Yazidi wakiwaita makafiri.

clouds stream