Urais 2015: Kamati kuu CHADEMA yajichimbia jijini Dar es salaam
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, inatarajia kujichimbia jijini Dar es samaa kuanzia Mei 3-4 kujadili uchaguzi mkuu wa rais na wabunge unaotarajia kufanyika wiki ya mwisho ya mwezi oktoba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene imebanisha kwamba katika kikao hicho cha siku mbili, pamoja na masuala mengine ya kitaifa kuhusu hali ya kisiasa nchini kwa ujumla na mengine mahsusi yanayohusu uendeshaji wa chama, KK itapokea taarifa, kujadili na kufanya maamuzi kuhusu;
- Maandalizi ya Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
- Taarifa ya ziara ya mafunzo kwa timu za kampeni, viongozi wa serikali za mitaa na chama, kukiandaa chama kushinda
dola na kuongoza serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. - Taarifa za utendaji wa chama kupitia kanda zote 10, Tanganyika na Zanzibar.
- Taarifa ya maendeleo ya mikakati ya kushiriki uchaguzi mkuu kwa kushirikiana na vyama 4 vinavyounda UKAWA.
- Taarifa za mwenendo wa shughuli ya uandikishaji wa wapiga kura (upya) katika daftari la kudumu kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) na hatma ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.