Sunday, 3 May 2015

Urais 2015: Mrema apingana na UKAWA

Urais 2015: Mrema apingana na UKAWA


Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema.
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema ameibuka na kuwapingana na kauli ya UKAWA dhidi ya kuhisi kuahirishwa uchaguzi mkuu kutokana na kutokamilika kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha,Mrema amesema  hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa kuongoza nchi kwa muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Katika mkutano wa UKAWA wiki iliyopita walidai kuwa Serikali na Tume ya Uchaguzi (NEC) inachelewesha uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura kwa lengo la kutaka kumwongezea Rais Kikwete muda wa kukaa Ikulu.
Mrema amebainisha kuwa yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutoa wazo la kutaka Rais Kikwete aongezewe muda zaidi wa kukaa Ikulu kwa kuwa kuna mambo mengi ambayo ni ya muhimu kwa Taifa yanayotakiwa kukamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu.
Mrema amesema alitoa maoni hayo mwaka jana wakati viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) walipokutana na Rais Kikwete mjini Dodoma, lakini alishangaa kuona viongozi wengine wakipinga wazo hilo.

clouds stream