Wednesday, 25 November 2015

Rais Kenyatta aongoza wananchi kumpokea Papa Francis

Rais Kenyatta aongoza wananchi kumpokea Papa Francis

Tarehe November 25, 2015
Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Papa Francis ambaye ni Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amewasili nchini Kenya leo na kupokewa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Ndege wa Kimaataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Ziara ya Kiongozi huyo mkubwa Duniani  kwa nchi ya Kenya inatarajiwa kuwa  siku tatu  kuanzia leo.
Alipotua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ( JKIA ), kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani alilakiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta.
Ziara ya Papa Francis nchini Kenya ni mwanzoni mwa ziara yake ya Afrika itakayomchukua pia hadi nchini Uganda na baadaye Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Kibadeni asema sasa ni kazi tu

Kibadeni asema sasa ni kazi tu

Tarehe November 25, 2015
Abdallah Kibaden
Abdallah Kibaden
Kocha wa Timu ya Taifa bara (Kilimanjaro Stars) Abdallah Kibadeni amesema kuwa atahakikisha timu yake inaendelea na kasi ya wimbi la ushindi katika michuano ya Chalenge na kusisitiza kikosi hicho kitakua kinafanya kazi Tu.
Kibadeni alisema hayo wakati akihjiwa na kituo cha televisheni cha Super Sport baada ya mechi kati ya Kilimanjaro Stars na Rwanda kumalizika kwa matokeo ya 2-1 ambapo Stars ilishinda mchezo huo.
Kibadeni alisema kuwa michuano ni migumu lakini aoni sababu ya timu yake kushindwa kutwaa ubingwa huo sababu anakikosi kizuri ambacho anakiamini.
katika mechi ya awali Stars ilitandika Somalia bao 4-0.

BOT yarejesha Chenji za Sarafu

BOT yarejesha Chenji za Sarafu

Tarehe November 25, 2015
Benki Kuu ya Tanzania.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imerejesha huduma ya chenji za sarafu ili kukidhi mahitaji ya chenji ya sarafu kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa huduma za Kibenki wa Benki kuu ya Tanzania (BOT), Martin Kobelo amesema hatua hiyo inafuatia kuadimika kwa sarafu ya shilingi 50, 100, 200,na 500 katika mzunguko wa fedha kwa watu na wafanyabiashara.
Amesema benki kuu imeanzisha dirisha la utoaji wa chenji za sarafu ambalo litaanza kufanya kazi kwa miezi sita ya mwanzo ili kuona kama uhitaji wa sarafu utaendelea kuwepo au utapungua.
<a href='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a08724c9&cb=Math.random()' target='_blank'><img src='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=19&source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&cb=Math.random()&n=a08724c9' border='0' alt='' /></a>
Akizungumzia utaoaji chenji Kobelo amesema huduma hiyo ya chenji sasa  itatolewa kikanda ambapo itatolewa na Benki kuu makao makuu na katika matawi yake ya Mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Zanzibar.
Kwa upande mwingine amesema kuwa huduma ya chenji ni bure kwa wananchi wote na hutolewa mara mbili kwa wiki, Jumanne na Alhamisi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.

clouds stream