Wednesday, 25 November 2015

BOT yarejesha Chenji za Sarafu

BOT yarejesha Chenji za Sarafu

Tarehe November 25, 2015
Benki Kuu ya Tanzania.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imerejesha huduma ya chenji za sarafu ili kukidhi mahitaji ya chenji ya sarafu kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa huduma za Kibenki wa Benki kuu ya Tanzania (BOT), Martin Kobelo amesema hatua hiyo inafuatia kuadimika kwa sarafu ya shilingi 50, 100, 200,na 500 katika mzunguko wa fedha kwa watu na wafanyabiashara.
Amesema benki kuu imeanzisha dirisha la utoaji wa chenji za sarafu ambalo litaanza kufanya kazi kwa miezi sita ya mwanzo ili kuona kama uhitaji wa sarafu utaendelea kuwepo au utapungua.
<a href='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a08724c9&cb=Math.random()' target='_blank'><img src='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=19&source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&cb=Math.random()&n=a08724c9' border='0' alt='' /></a>
Akizungumzia utaoaji chenji Kobelo amesema huduma hiyo ya chenji sasa  itatolewa kikanda ambapo itatolewa na Benki kuu makao makuu na katika matawi yake ya Mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Zanzibar.
Kwa upande mwingine amesema kuwa huduma ya chenji ni bure kwa wananchi wote na hutolewa mara mbili kwa wiki, Jumanne na Alhamisi kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana.

clouds stream