CCM wajitokeza Kuzungumzia Kasi ya Rais Magufuli
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejitokeza kwa mara ya kwanza na Kumpongeza Rais John Magufuli katika utendaji wake tangu aingie madarakani mapema novemba,2015.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema kuwa CCM inamuunga mkono hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Rais John Magufuli za kutumbua majipu.
Wamempongeza kwa kubana matumizi ya umma, kuziba mianya ya rushwa, kupiga vita ubadhirifu wa mali ya umma na kurejesha nidhamu na uwajibikaji kwenye taasisi za umma na nchi kwa ujumla.
Wenyeviiti hao wamemuomba Rais Magufuli aendeleze kasi yake ya kutekeleza majukumu yake na asisite kuwawajibisha watendaji wote wazembe wanaozalisha kero ya utoaji huduma duni kwa wananchi.
Madabida alisema katika kampeni zilizoendeshwa kote nchini, Dk Magufuli aliahidi Watanzania watakapomchagua kuwa Rais atatekeleza kwa juhudi na maarifa masuala ya kuondoa umasikini; kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana; kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma na kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama kwa maisha ya wananchi na mali zao. Kwa upande mwingine wenyeviti hao wamefadhaishwa na vitendo vya vilivyofanywa na wabunge wa kambi ya Upinzani vya kupiga kelele na kusababisha kutolewa nje kabla ya Dk Magufuli kutoa hotuba yake Bungeni hivi karibuni.