Tuesday, 22 December 2015

Kasi Ya Rais Magufuli Yatua Rwanda, Kagame Afunguka

Kasi Ya Rais Magufuli Yatua Rwanda, Kagame Afunguka

Tarehe December 22, 2015
Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais wa Rwanda Paul Kagame   amefunguka kwa mara ya kwanza mara baada ya rais John Magufuli kuingia Ikulu Novemba 5 mwaka 2015.
Kwa mujibu wa Balozi wake nchini, Uegene Kayihura amesema kwamba Rais Kagame amefurahishwa na hatua ambazo Rais John Magufuli anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa bandari.
Kayira amesema hayo alipofika Ikulu ya Rais Magufuli  ambapo  amemhakikishia kuwa Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania, hasa katika kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kwa  kuwa Rwanda inapitisha asilimia 70 ya mizigo yake katiba Bandari ya Dar es salaam.
Ameongeza kuwa  Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua kusafisha uozo katika bandari, kufichua ufisadi wa mabilioni ya shilingi kutokana na upotevu wa makontena, ambayo hayakulipiwa kodi stahili kwa serikali, kuvunjwa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadhi Massawe na kusimamisha maofisa kadhaa wa bandari hiyo na wengine wanaohusika na usimamizi wa bandari kavu.
Katika kuimarisha utendaji Bandarini  na Mamlaka ya Mapato Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade na maofisa wengine wa mamlaka hiyo, ambao miongoni mwao tayari wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutokana na ubadhirifu huo.

clouds stream