Monday, 7 December 2015

Kasi ya Rais Magufuli yawatimua Vigogo 7 Tanecso

Kasi ya Rais Magufuli yawatimua Vigogo 7 Tanecso

Tarehe December 6, 2015
Makao makuu ya Shirika la Umeme Tanzania.
Makao makuu ya Shirika la Umeme Tanzania.
Kasi ya Rais John Pombe Magufuli ime endelea kushika kasi katika kuwashughulikia watendaji wazembe ambapo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewatimua kazi  wafanyakazi 7 kutokana na makosa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Tanesco imebainisha kuwa imewachukulia hatua wafanyakazi ambao wamekuwa wakitoa huduma  mbaya na kuwa Kero kwa wateja zikiwemo lugha mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma, kucheleweshewa huduma na ubadhirifu.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.
Aidha, Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na kuripotiwa na vyombo vya habari jana. Walioachishwa kazi ni pamoja na wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, Wahandisi na Wahasibu.


Taarifa hiyo imesisitiza kuwa  Shirika linaendelea na uchunguzi na mfanyakazi ye yote atakayebainika analaghai wateja, anadai rushwa, anatoa lugha chafu au huduma mbovu atawajibishwa mara moja na pale atakabobainika    ataachishwa kazi.
Kwa upande mwingine shirika hilo limesema kwamba ili kuendana na agizo la Rais Magufuli la kufanya usafi Desemba 9 nchini Wafanyakazi wote wa TANESCO watashiriki katika shughuli mbali mbali za usafi wa mazingira katika maeneo yote yanayozunguka ofisi, mitambo na vituo nchi nchi nzima.

clouds stream