Monday, 15 May 2017

KITWANGA ADAI ALI - BEEP TU , MAZITO YANAKUJA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga.
Charles Kitwanga.
IMG-20170426-WA0006

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema kuwa yale aliyochangia bungeni katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ni kama ali­‘beep’ tu na kwamba mazito yanakuja bila kuweka bayana mazito hayo.

Kitwanga ambaye ni Mbunge wa Misungwi (CCM) amesema hayo kufuatia majibu makali yaliyotolewa na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge aliyemtaka Kitwanga ahame chama cha CCM kama anaona haridhiki na utendaji wake.

Hivi karibuni wakati akichangia mjadala wa bajeti hiyo, Kitwanga alitishia kuwahamashisha wananchi 10,000 wa jimbo lake kwenda kuzima mtambo wa maji wa Kijiji cha Ihelele kutokana na kijiji hicho kutopata maji katika chanzo hicho.

Akijibu hoja hiyo, Waziri Lwenge aliifananisha nia hiyo kama uasi na kuonyesha kuwa kama hathamini na haridhiki na kazi inayofanywa na chama chake basi ahame. Sasa hivi mimi ni mbunge, nina wajibu wa kuhoji.

Nawaambia siku ile nili­beep, sasa nitapiga kabisa. Watatambua kuwa nilipokuwa kijana nilikuwa mwanaharakati lakini sasa uharakati ndio umezidi.

clouds stream