Thursday, 18 May 2017

KIKWETE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI MWENZA BARAZA LA WAKIMBIZI DUNIANI

jk1
Rais wa Awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete

IMG-20170426-WA0006

Aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza katika Baraza Kuu la Wakimbizi duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi wanaolenga kubuni mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi. 

Taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari vimemtaja bwana Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo chini ya uenyekiti wa waziri wa maswala ya kigeni nchini Canada Lloyd Axworthy.

Baraza hilo litaleta mabadiliko ili kusadia na kuhakikisha kuwa ushirikiano wa kimataifa kwa wakimbizi unaeleweka,unafanyika kwa njia ya usawa na haki

clouds stream