Friday 26 May 2017

Simu Mpya Za Kisasa Za Nokia 3310 Zaingia Madukani

_94853899_001

IMG-20170426-WA0006

Simu za Nokia 3310 zimeanza kuuzwa tena madukani, takriban miaka 17 baada ya simu hizo kuanza kuuzwa mara ya kwanza.

Simu za sasa zina kamera ya megapikseli mbili na zinategemea teknolojia ya 2.5G kumpa mteja huduma ya kiwango cha chini sana cha mtandao wa Intaneti.

Simu hiyo inauzwa £49.99 (Dola 65). Betri za simu hizo zinadaiwa kudumu kwa saa 22 mtu akiitumia kuzungumza, na inaweza kukaa na chaji kwa hadi mwezi mmoja iwapo mtu hatakuwa anaitumia.

Mtaalamu mmoja amesema ufanisi wa simu hiyo utategemea sana hamu ya watu kutaka kulipia kifaa hicho ambacho wengi bado hukikumbuka kwa mazuri yake.

Watu wengi walizipenda sana simu za Nokia 3310 kutokana na uthabiti wake na uwezo wa kukaa na chaji.

“Kwa mtu kama mimi, siku ya leo ni ya furaha sana,” amesema Ben Wood, kutoka kwa kampuni ya masuala ya teknolojia ya CCS Insight.

“Ukiweka simu hii mikononi mwa mtu aliyebalehe karne ya 21 ambaye uraibu wake ni kukaa Snapchat, bila shaka utakuwa umekosea,” ameongeza.

clouds stream