Wednesday, 24 May 2017

JPM Amtaka Profesa Muhongo Kuachia Ngazi

Profesa-Sospeter-Muhongo
IMG-20170426-WA0006
Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ajipime, ajifikirie na haraka sana aachie ngazi kufuatia ripoti ya Tume Maalum iliyoundwa na Rais Magufuli kuchunguza makontena 277 ya makinikia yanayoshikiliwa iliyowasilishwa leo Ikulu.
“Profesa Muhongo ni rafiki yangu lakini kwa hili ajifikirie, ajipime na ningependa ajiuzulu mara moja,” amesema Rais Magufuli aliyeoneka kukasirishwa na ripoti hiyo.
Amesema mapendekezo yote tisa yaliyopendekezwa na kamati hiyo yamekubaliwa na kuivunja maramoja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kuagiza vyombo vya dola vikishirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuanza kuwafatilia wafanyakazi wote wa TMAA kwa ajili ya hatua za kisheria kuanzia leo.
“Inaumiza sana kuona tunapambana kutafuta pesa hata kwa kukopa, kumbe kuna hela tumeziacha zinamwagika huko, inaumiza sana,” amesema Rais Magufuli.
Aidha, ameagiza vyombo vya dola na TAKUKURU kuwachunguza baadhi ya watendaji wa Wizara ya Madini waliokuwa wakihusika na madini na kumtaka, Kamishna wa Madini wa Zamani na kuwachukulia hatua mara moja.
Awali akiwasilisha ripoti hiyo mbele ya Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema Serikali inapoteza kati ya Shilingi 829.4 bilioni na Sh1.439 trilioni wakati wa kusafirisha makinikia nje ya nchi.
Prof Mruma amemkabidhi Rais Magufuli ripoti ya uchunguzi wa kiwango, aina ya madini kwenye makontena 277 ya makinikia yanayoshikiliwa.

clouds stream