Friday 26 May 2017

SERIKALI YAWAPA AHUENI WANANCHI KUMILIKI ARDHI

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi.
IMG-20170426-WA0006

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetangaza kupunguza tozo ya mbele ya thamani ya ardhi kutoka asilimia 7.5 hadi 2.5 kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema hayo Bungeni Dodoma jana wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2017/18.

Katika hotuba yake Lukuvi alisema punguzo hilo ni sawa na asilimia 67 ya tozo hiyo, hali itakayowasaidia wananchi kumiliki mashamba na viwanja vilivyopimwa.

Alisema lengo la kufuta tozo hizo ni kuwezesha wengi kumiliki maeneo yao kwa gharama nafuu na kupanua wigo wa walipa pango la ardhi.

“Ada hii hutozwa mara moja wakati wa umilikishwaji ardhi kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999. Kupunguzwa kwake kutavutia wananchi wenye maeneo ya ardhi kujitokeza kwa wigi zaidi kupimiwa viwanja na kumilikishwa ardhi yao,” alisema.

Alisema pia kupunguzwa kwa tozo hiyo kutapunguza gharama kubwa za sasa za viwanja na kufanya wengi kumudu kumiliki viwanja vilivyopimwa

clouds stream