Tuesday, 23 May 2017

Trump kukutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas

Trump kukutana na kiongozi wa Palestina

Trump kukutana na kiongozi wa Palestina

IMG-20170426-WA0006

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kukutana na kiongozi wa utawala wa palestina Mahmoud Abbas wakati wa siku ya pili ya ziara yake Mashariki ya Kati

Waisrael na wapalestina hawajafanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa zaidi ya miaka mitatu.

Siku ya Jumatatu Trump alisema kuwa kuna ushirikiano mkubwa kati ya Marekani na Israel

Pia alionya juu ya kuwepo kwa tisho la Iran kwa amani ya dunia

Waandamanaji walirusha mawe kupinga ziara ya Trump huko Ukingo wa Magharibi siku ya Jumatatu
Waandamanaji walirusha mawe kupinga ziara ya Trump huko Ukingo wa Magharibi siku ya Jumatatu

Alimuambia waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa kamwe Iran haitaruhusiwa kumiliki silaha za nuklia.

Ziara huiyo ya siku mbili nchini Israel na katika utawala wa Palestina ni sehemu ya ziara ya ya kwanza ya kigeni ya bwana Trump.

Rais Trump anajitambua kama mpatanishi mkuu wa kutatua masuala ambayo yamewashinda watu wengi.

Suala kuu ni kubuniwa kwa taifa huru la palestina kando ya Israel.

Baadhi ya wapalestina huko Gaza walipinga ziara ya Trump
Baadhi ya wapalestina huko Gaza walipinga ziara ya Trump

Eneo la ukingo wa Magharibi pamoja na mashariki mwa mji wa Jerusalem limekaliwa na Israeli kwa miaka 50.

Baadhi ya watu wenye ushawishi ndani ya serikali ya Israel wanaamini kuwa ardhi hiyo ni ya Waisraeli waliyopewa na Mungu.

Utawala wa Palestina umegawanyika huku Kundi la Fatah likitawala huko Ukingo wa Magharibi na Hamas huko Gaza.

clouds stream