Thursday, 2 April 2015

Simba yaingia mkataba ‘mnono’ na EAG Group Limited

Simba yaingia mkataba ‘mnono’ na EAG Group Limited


Makamu wa Rais wa klabu ya Simba SC Godfrey Nyange ‘Kaburu’ akifafanua jambo
Klabu ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba, leo imeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya EAG Group Limited ambao utahusika na masuala ya kuitafutia dili za kuiingiza pesa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi wa EAG Imani Kajula amesema kuwa, mipango yote ya kuendesha dili hilo anaipata kutoka katika Klabu ya Arsenal ya England ambayo anafanya nayo kazi.
Kajula amesema katika mkataba huo anataka kuiona Simba inakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato ili iache kutegemea mapato ya mlangoni na ada ya wanachama pekee.
Naye rais wa klabu hiyo Evans Aveva amesema, anaamini mpango huo utawawezesha kuendeleza jengo lao la makao makuu liliopo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar.
Aidha katika hatua nyingine, klabu hiyo imetangaza kuwa kila mwisho wa msimu itakuwa inamtangaza mchezaji wao bora wa klabu kwa mwaka ambapo atazawadiwa zawadi ya gari la kisasa huku mchezaji bora kijana akipewa pesa shilingi milioni tano na mchezaji mwenye nidhamu atapokea milioni mbili.
Amesisitiza kuwa washindi hao wote kila mmoja pia atazawadiwa simu ya kisasa aina ya Huawei Ascend Mate 7 yenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kutoka kampuni ya Huawei ambayo wameingia udhamini na klabu hiyo.

Mjomba afukua kaburi la Ndugu yake mwenye ualbino na Kuiba mifupa

Mjomba afukua kaburi la Ndugu yake mwenye ualbino na Kuiba mifupa


Watu wawili  akiwemo mjomba wa marehemu ajulikanaye kama  January Korongo wamekatwa na Jeshi la Mkoani Kagera kwa tuhumza za kufukua kaburi la mtu mwenye ulemavu wa ngozi albino aliyefariki dunia mwaka 1991 na kuchukua mifupa yote iliyokuwemo katika jeneza kwa lengo la kuiuza.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Laston Faustine (41), ambaye ni mkazi wa Lukulaijo aliyekutwa na mfuko uliokuwa umehifadhi mifupa mitatu ya binadamu na mwingine ni January Korongo (43), mkazi wa Kadengesho, wiyani Karagwe.
Watu hao walikamatwa Machi 27, mwaka huu, katika nyumba moja ya kulala wageni, iliyoko eneo la Kyaka, Wilaya ya Missenyi baada ya kukutwa wakiwa na baadhi ya viungo hivyo, ambavyo walikuwa wanakwenda kuviuza walivovitoa katika jeneza mwaka 2009.
Mwaibambe alisema baada ya kumhoji zaidi mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na polisi hadi nyumbani kwake, ambako alionyesha fuvu la kichwa, mifupa mitatu ya miguu pamoja na mifupa ya sehemu mbalimbali, ambayo ilikuwa imefungwa kwenye mfuko nje ya nyumba yake.
Hata hivyo jeshi la polisi lilifanikiwa kufukua kaburi hilo na kukuta viungo vyote vimetolewa.
Watuhumiwa hao wote wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo hivi karibuni.

Mambo 10 usiyojua kutoka kwa Rais mpya wa Nigeria

Mambo 10 usiyojua kutoka kwa Rais mpya wa Nigeria


Taifa kubwa barani Afrika Nigeria limemaliza mchakato wa urais huku ushindi wa kishindo wa Muhammadu Buhari akimuangusha Goodluck Jonathan kwa kura milioni 15.4 kwa kura za mpinzani wake Goodluck Jonathan ambaye alipata kura milioni 12.9. Hapa inaonekana wananchi wa Nigeria wameona wachagua rais mwingine ambaye ataweza kubadilisha hali ya machafuko nchini humo yanayofanywa na Boko Haram ambaye Rais aliyekuwepo Goodluck Jonathan alishindwa.

Akihojiwa mara baada ya kutangazwa mshindi wa Urais nchini Nigeria Rais Muhammadu Buhari alisema maeneno machache ambayo ni ushindi wake huo ni wa wananchi wote wa Nigeria.
Mambo 10 usiyoyajua kutoka kwa Rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari;
-Ana miaka 72
-Rais wa kwanza wa Nigeria kutoka chama cha upinzani
-Muislamu kutoka kaskazini mwa Nigeria
-Alikuwa kiongozi wa Jeshi kuanzia 1984-1985
-Ana rekodi mbaya ya haki za binadamu
-Mtu anaependa sana nidhamu kazini
-Alitoroka kwenye mauaji ya Boko Haram
– Sio mpenda Rushwa
-Ameshinda uchaguzi kwa tofauti ya kura milioni 2.1
Rais wa kwanza wa Nigeria kutoka chama cha Upinzani

clouds stream