Mjomba afukua kaburi la Ndugu yake mwenye ualbino na Kuiba mifupa
Watu wawili akiwemo mjomba wa marehemu ajulikanaye kama January Korongo wamekatwa na Jeshi la Mkoani Kagera kwa tuhumza za kufukua kaburi la mtu mwenye ulemavu wa ngozi albino aliyefariki dunia mwaka 1991 na kuchukua mifupa yote iliyokuwemo katika jeneza kwa lengo la kuiuza.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Laston Faustine (41), ambaye ni mkazi wa Lukulaijo aliyekutwa na mfuko uliokuwa umehifadhi mifupa mitatu ya binadamu na mwingine ni January Korongo (43), mkazi wa Kadengesho, wiyani Karagwe.
Watu hao walikamatwa Machi 27, mwaka huu, katika nyumba moja ya kulala wageni, iliyoko eneo la Kyaka, Wilaya ya Missenyi baada ya kukutwa wakiwa na baadhi ya viungo hivyo, ambavyo walikuwa wanakwenda kuviuza walivovitoa katika jeneza mwaka 2009.
Mwaibambe alisema baada ya kumhoji zaidi mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na polisi hadi nyumbani kwake, ambako alionyesha fuvu la kichwa, mifupa mitatu ya miguu pamoja na mifupa ya sehemu mbalimbali, ambayo ilikuwa imefungwa kwenye mfuko nje ya nyumba yake.
Hata hivyo jeshi la polisi lilifanikiwa kufukua kaburi hilo na kukuta viungo vyote vimetolewa.
Watuhumiwa hao wote wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo hivi karibuni.