Monday, 26 May 2014

DIEGO SIMEONE AKIRI MAKOSA.


Kocha Mkuu wa Atletico Madrid Diego Simeone amekiri kuwa alifanya makosa kumpanga Diego Costa katika mechi ya fainali baina ya timu hiyo na Real Madrid.
Real Madrid hapo jana iliibamiza Atletico Madrid kwa jumla ya magoli 4 - 1 na kunyakua kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya."Hakuna mashaka kiwango alichoonyesha Diego uwanjani nina wajibu wangu nilifanya makosa lazima nikubali," Kocha Simeone alisema.Costa alibadilishwa baada ya kuumia msuli wa paja ikiwa zimebaki dakika 9 mechi hiyo imalizike.
Mshambuliaji huyo raia wa Hispania aliumia alipocheza mechi baina ya Atletico na Barcelona wiki moja iliyopita na ameweza kuifungia magoli 36 timu katika msimu huu.
Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Brazil alionekana kuwa chini ya kiwango na alibadilishwa na Adrian Lopez.
"Sitaki kupoteza muda tulicheza pungufu mchezaji mmoja", Kocha huyo alisema.

UCHAGUZI WA MALAWI KUBATILISHWA.


Uchaguzi wa Malawi wabatilishwa

Vyombo vya habari vimemnukulu mkuu wa tume ya uchaguzi Maxon Mbendera akisema kuwa mchakato wa kuhesabu kura utaendelea na kwamba rais hana mamlaka ya kubatilisha uchaguzi rasmi.
Rais wa Malawi Joyce Banda
Rais wa Malawi Joyce Banda ilipohaririwa mwisho 24.05.2014 16:06Rais wa Malawi Joyce Banda amebatilisha uchaguzi wa urais uliofanywa wiki hii kutokana na kasoro za masanduku ya kura, lakini maafisa wa uchaguzi mara moja wakapinga maamuzi yake.

Akizungumza na waandishi habari Jumamosi, rais Banda alisema ana mamlaka kikatiba kubatilisha kura hiyo na kuelezea kwamba matukio kadhaa  ikiwemo uingiliaji kati wa masanduku ya kura na kuongezewa  kwa masanduku ya kura yasiyo halali kumesababisha achukue hatua hiyo.

Bi Banda pia amesema uchaguzi mwingine utafanyika ndani ya siku 90, na kwamba yeye hatagombea urais.

Alisema alitumaini kushinda uchaguzi huo na kuongoza Malawi kwa  muhula mwingine, baada ya kuliongoza taifa hilo kwa miaka miwili kufuatia kifo cha mtangulizi wake Bingu wa Mutharika.

Vyombo vya habari vimemnukulu mkuu wa tume ya uchaguzi Maxon Mbendera akisema kuwa mchakato wa kuhesabu kura utaendelea kufuatia uchaguzi wa Jumanne wiki hii na kwamba rais hana mamlaka ya kubatilisha  uchaguzi rasmi.

Friday, 23 May 2014

HOUSE FOR SALE AT SINZA MAKANYA.

LOCATION: SINZA MAKANYA

FEATURES: 3 BEDROOMS, DINNING AND KITCHEN- FENCED

PRICE: TSH 65 MIL

CONTACT: +255 652 314 181

EMAIL: nijuzetz@gmail.com





clouds stream