TMA : Tanzania kukumbwa na ukame 2015
Kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa TMA, Agnes Kijazi amesema kwamba kufuatia hali ya ukame kutokea mwaka huu, huenda ika athiri uzalishaji wa umeme kutokana na nchi ya Tanzania kutegemea maji kama chanzo cha nishati.
Upungufu wa unyevu ardhini, ukosefu wa mvua umetajwa kuathiri shughuli za kilimo katika maeneo mengi nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutoa mwelekeo wa mvua za masika kwa marchi, April na Mei mwaka huu Kijazi amesema mvua za wastani na juu ya wastani, zitanarajiwa katika baadhi ya maeneo hususani Kanda ya Ziwa Victoria na maeneo ya Kusini.
Kwa upande wa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua, mvua zinatarajia kuanza mapema na kutakuwepo kwa vipindi vya ukame katika maeneo mengi hususani machi na Mei.