UVCCM yamuonya Nape ‘kumponda’ Lowassa
Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoani Arusha, umemuonya katibu wa itikadi na
uenezi Nape Nnauye kuchunga kauli zake kufuatia kauli aliyoitoa dhidi
ya Edward lowassa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) MKoani Arusha, Robson Meitinyiki amesema Nape anapaswa kuelewa chama hicho kilibomoka na kuwa ni chama cha watu wote na kwa sasa chama kimeanza kuimarika kupitia jitihada za Katibu Mkuu, Abdurahamani Kinana na yeye anaanza kujinyanyua na kutaka kukibomoa.
Ameongeza kuwa Nape aelewe nyuma ya Lowassa wapo wengi na Arusha wanajipanga kwenda kumshawishi achukue fomu na yeye hapaswi kutoa maneno ya kejeli, kwani kuna kanuni na taratibu za vyama vya kumsimamisha mtu kuwa mgombea, kama ana mgombea wake amtangaze japo lazima apitishwe na chama,siyo mtu mmoja.
Kwa upande wake Katibu Mwenezi Mkoa wa Arusha, Isack Joseph, amesema Nape afike mahali achunge kauli zake dhidi ya Lowassa, kwani Lowasa ni mtu mwenye heshima katika nchi hii na alikuwa Waziri Mkuu na kuiletea taifa heshima kubwa.
Kwa upande mwoingine Robson amesema kama Edward Lowassa anafanya maigizo, ili apendwe na watu, basi wanamshauri mgombea wa Nape afanye maigizo hayo, ili apendwe na watu kwa kufuatwa nyumbani kwake.