Sakata la Escrow: Wahisani wakubali kuimwagia Tanzania mabilioni ya fedha
Wafadhili mbalimbali kutoka nje ya nchi watanatarajia kutoa kiasi cha shilingi bilioni 784 ambazo ni asilimia 85 ya fedha zilizobaki kukamilisha bajeti ya mwaka wa huu wa fedha.
Hatua ya wafadhili kutoa kiasi hicho cha fedha inafuatia kuridhishwa na masharti waliyotoa waki itaka serikali serikali ya Tanzania kuwachukulia hatua vigogo serikalini waliopelekea kupotea kwa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow mwaka jana.
Kwa mujibu wa waziri wa fedha Saada Mkuya akizungumzia utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na wafadhili katika kusaidia bajeti ya serikali mwaka huu, amesema wafadhili hao ikiwemo nchi ya Finland wataanza kutoa dola milioni 44 za Marekani hivi karibuni.
Katika hatua nyingine Mkuya amesema serikali inaendelea kurejesha mahusiano mazuri na wahisani suala litakalo pelekea waendelee kutoa fedha za kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo nchini inayotegemea fedha za wahisani.