Zitto atoa ya Moyoni kufuatia kuvuliwa uanachama CHADEMA
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ametoa ya moyoni kufuatia kuvuliwa uanachama CHADEMA. Hatua ya kuvuliwa uanachama wa chama hicho unafuatia Mwanasheria mkuu wa CHADEMA,Tundu Lissu kutangaza rasmi jana kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Aidjha, akifafanua jambo hilo Tundu Lissu amesema iwapo mwanachama atafungua kesi dhidi ya chama na iwapo atashidwa atakuwa amejiondoa mwenyewe. Mwaka jana Zitto alifungua kesi Mahakama kuu akipinga kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kumjadili, akikitaka chombo hicho cha sheria, kukielekeza chama chake, kusubiri kwanza rufaa yake aliyokuwa amekata katika Baraza Kuu.
Baada ya kupata taarifa hizo Zitto amesema kuwa hakuwa na wito wa mahakamani jana na Jaji aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo amehamishiwa Tabora, hivyo mwanasheria wake ameenda kufuatilia mazingira ya hukumu hiyo.
“Hatuna taarifa ya Jaji Mpya. Mwanasheria wetu anafuatilia na atatoa statement”, ameandika Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa twitter.
Ujumbe aliouandika Zitto Kabwe katika ukurasa wake wa twitter.