Sakata la Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama lachukua sura mpya
Sakata la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama Chadema limechukua sura mpya kufuatia chama cha Chadema kutomwandikia barua ya kuvuliwa uanachama mbunge huyo suala linalopelekea kuendelea na shughuli zake kamati kama kawaida.
Bunge linasemaje kuhusiana na sakata hilo,
Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema kwamba haijapata barua yeyote kuhusu kuvuliwa uanachama wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Kwa mujibuwa katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashililah amesema kwamba kwa kuwa bado hawajapa barua kutoka Chadema Zitto bado ni Mbunge halali wa Kigoma na anatakiwa kuendelea na shughuli kama kawaida.
Ameongeza kuwa ikiwa Bunge litapata Barua ya kuvuliwa uanachama, Bunge litafanya uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo zinazo mkabili ndipo litoe uamuzi. Hata hivyo amesema si lazima spika akubaliane na uamuzi wa kutengua ubunge wa Mbunge husika kwani kama haikuwa halali kuvuliwa uanachama Spika hubatilisha uamuzi wake wa kumvua ubunge mhusika.
Naye Ofisa Hbari wa Chadema Tumaini Makene amesema chama hicho kitajitahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa kuzingatia sheria na taratibu pamoja na kuandaa barua hiyo kwa wakati.
Katika hatua nyingine Zitto amesema anachukulia suala la kuvuliwa uanachama kama changamoto ambayo inazidi kumkuza na kumkomaza katika tasnia ya siasa ndani na nje ya nchi.